• HABARI MPYA

    Monday, September 18, 2023

    ABDALLAH KHERI WA AZAM FC AFANYIWA UPASUAJI WA GOTI AFRIKA KUSINI


    BEKI wa kati wa Azam FC, Abdallah Kheri 'Sebo', atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti lake la mguu wa kulia.
    Sebo ameumiza gegedu 'cartilage' ya maungio ya goti lake la mguu wa kulia, ambayo imelika na pia ameumiza mifupa midogo midogo kutokana na mlalo wa goti lake la kulia na tege alilokuwa nalo.
    Beki huyo kisiki, amefanyiwa upasuaji huo leo Jumatatu asubuhi, kwenye Hospitali ya Vincent Palloti, jijini Cape Town, Afrika Kusini.
    Abdallah Kheri ‘Sebo’ aliumia kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tanzania Prisons, Azam FC ikishinda mabao 3-1 na kushindwa kuendelea wakati wa mapumziko nafasi yake ikichukuliwa na Nathan Chilambo.
    Daktari wa Azam FC, Dr. Mwanandi Mwankemwa, aliyeambatana na beki huyo, amesema kuwa Sebo atarejea kwenye soka la ushindani baada ya miezi mitatu ya matibabu ya majeraha yake kumalizika.
    "Sebo amefanyiwa upasuaji wa kisasa unaoitwa arthroscopic, ambao wametoa mifupa midogo midogo iliyokuwa imevunjika na kupandikiza gegedu nyingine.
    "Baada ya kufanyiwa upasuaji huo, mchezaji ameelekezwa mazoezi ya kufanya kwa muda wa mwezi mzima na anatakiwa kupumzika kwa muda wa miezi mitatu," alisema Dr. Mwankemwa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ABDALLAH KHERI WA AZAM FC AFANYIWA UPASUAJI WA GOTI AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top