• HABARI MPYA

  Saturday, September 16, 2023

  YANGA YAWANYAMZISHA MERREIKH KWA KICHAPO CHA 2-0 KIGALI


  MABINGWA wa Tanzania, Yanga wametanguliza mguu mmoja hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya El Merreikh ya Sudan jioni ya leo Uwanja wa Pele Jijini Kigali, Rwanda leo.
  Mabao ya Yanga katika mchezo huo wa kwanza wa Hatua ya 32 Bora yamefungwa na washambuliaji wake, Mzambia, Kennedy Musonda dakika ya 60 na mzawa, Clement Mzize dakika ya 79.
  Timu hizo zitarudiana Jijini Dar es Salaam Jumamosi ijayo na mshindi wa jumla atakwenda hatua ya 16 Bora ambayo itachezwa kwa mfumo wa makundi.
  El Merreikh wamelazimika kutumia Uwanja wa Pele kama wa nyumbani kutokana na machafuko yanayoendelea Sudan.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAWANYAMZISHA MERREIKH KWA KICHAPO CHA 2-0 KIGALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top