• HABARI MPYA

  Saturday, September 09, 2023

  MABONDIA SITA WA TANZANIA KUWANIA TIKETI YA OLIMPIKI

  TMU ya Taifa ya Ngumi ya Tanzania "Faru weusi wa Ngorongoro" imewasili salama jana jioni katika Jiji la Dakar, Senegal tayari kwa mashindano ya kufuzu Olimpiki ya Paris 2024 kwa Bara la Afrika. 
  Jumla ya mabondia 6 kuiwakilisha Tanzania chini ya Mwalimu Mkuu Samwel Beatmen Kapungu (IBA 1star) ambao ni Kapteni na mshindi wa Medali ya Shaba Jumuiya ya Madola 2022 na Afrika 2023 Yusuf Changalawe 80kg, Mwalami Mohamed 57kg, Abdallah Abdallah "Katoto" 51kg, Musa Maregesi 92kg, Zulfa Macho 50kg na Mshindi wa Medali ya Fedha Afrika 2023 Grace Mwakamele 66kg.
  Mashindano haya yanayoanza rasmi leo tarehe 9-15 September, 2023, yanashirikisha jumla ya mabondia 250 wanaoziwakilisha kamati za Olimpiki 43 za Mataifa ya Afrika kuwania nafasi 18 za awali za kufuzu Olimpiki ya Paris 2023 kwa Bara la Afrika.
  Raisi wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa Shirikisho la Ngumi Afrika (AFBC) Ndg. Lukelo Willilo ameongozana na timu kama mkuu wa msafara pamoja na Katibu Mkuu Ndg. Makore Mashaga na mjumbe wa kamati ya maendeleo ya vijana na wanawake BFT Bi. Asha George. 
  Tanzania itaanza kupeperusha bendera leo kutafuta tiketi za kushiki Olimpiki 2024 kwa mapambano yafuatayo 
  Bout no. 1 
  Zulfa Macho vs Grace Nankinga kutoka Uganda. 
  Bout no. 3 
  Abdallah Abdallah "Katoto" vs Patrick Gomes Fernandez kutoka Visiwa vya Cape Verde.
  Bout no. 30 
  Mwalami Mohamed vs Idris Kabwe Kitangila kutoka DR Congo
  Mungu ibariki Tanzania 🇹🇿 🥊
  Imetolewa na: 
  Ofisi ya Raisi - BFT


  📸 Kutoka kushoto Musa Maregesi, Zulfa Macho, Abdallah "Katoto", Mwalami Mohamed na Yusuf Changalawe baada ya kuwasili tu katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Blaise Diagne Dakar na Ndege ya Ethiopia Airlines kupitia Addis Ababa na Bamako.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MABONDIA SITA WA TANZANIA KUWANIA TIKETI YA OLIMPIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top