• HABARI MPYA

  Saturday, September 16, 2023

  MANCHESTER CITY WAICHAPA WEST HAM 3-1 LONDON


  MABINGWA watetezi, Manchester City wametoka nyuma na kuwachapa wenyeji, West Ham United mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa London.
  West Ham ilitangulia na bao la dakika ya 36 la James Ward-Prowse, kabla ya Manchester City kuzinduka na mabao ya J. Doku dakika ya 46, Bernardo Silva dakika ya 76 na Erling Haaland dakika ya 86.
  Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 15 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi mbili zaidi ya Tottenham Hotspur na Liverpool, wakati West Ham inabaki na pointi zake 10 nafasi ya sita baada ya wote kucheza mechi tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANCHESTER CITY WAICHAPA WEST HAM 3-1 LONDON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top