• HABARI MPYA

  Thursday, September 28, 2023

  NI MAN UNITED NA NEWCASTLE 16 BORA CARABAO CUP


  TIMU ya Manchester United itakutana na Newcastle United katika mchezo wa Hatua ya 16 Bora Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup Oktoba 30 Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Hayo yatakuwa marudio ya mchezo wa Fainali ya Carabao Cup msimu uliopita, Mashetani Wekundu walipoichapa Newcastle 2-0 Uwanja wa Wembley na kubeba taji hilo.
  Mechi zote za 16 Bora Carabao Cup zitachezwa Oktoba 30 na Liverpool watawafuata AFC Bournemouth, Arsenal watawafuata West Ham United, wakati Chelsea watawakaribisha Blackburn Rovers.
  RATIBA HATUA YA 16 BORA CARABAO 
  Manchester United v Newcastle
  Chelsea v Blackburn 
  Bournemouth v Liverpool 
  Everton v Burnley 
  West Ham v Arsenal
  Mansfield Town v Port Valer
  Exeter City v Middlesbrough 
  Ipswich Town v Fulham 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI MAN UNITED NA NEWCASTLE 16 BORA CARABAO CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top