• HABARI MPYA

  Friday, September 15, 2023

  TABORA UNITED YAWATANDIKA TANZANIA PRISONS 3-1 MWINYI


  TIMU ya Tabora United imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora.
  Mabao ya Tabora United, zamani Kitayosce yamefungwa na John Ben dakika ya 42 na 90 na ushei na Eric Okutu dakika ya 58, wakati bao pekee la Tanzania Prisons limefungwa na Samson Mbangula dakika ya 70.
  Tabora United inafikisha pointi nne, wakati Tanzania Prisons inabaki na pointi yake moja baada ya wote kucheza mechi tatu. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TABORA UNITED YAWATANDIKA TANZANIA PRISONS 3-1 MWINYI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top