• HABARI MPYA

    Sunday, September 10, 2023

    CHANGALAWE AMTWANGA MKONGO NA KUTINGA ROBO FAINALI KUFUZU OLIMPIKI 2024


    BONDIA Yusuf Changalawe wa Tanzania amefanikiwa kutinga Robo Fainali ya Mashindano ya kufuzu Michezo ya Olimpiki ya mwakani Jijini Paris kwa Afrika baada ya kumshinda Mpi Anauel Ngamissengue wa Kongo Brazzaville  kwa points 5-0 uzito wa Light Heavy leo Jijini Dakar nchini Senegal.
    Kwa ushindi huo, Changalawe ameingia hatua ya robo fainali ya mashindano ya kufuzu Paris Olimpiki 2024 yanayoendelea katika Jiji la Dakar, Senegal ambapo jumla ya  nafasi za awali 18 za kufuzu kushiriki Olimpiki kwa Bara la Afrika zinagombewa.
    Awali ya hapo, Zulfa Macho Yussuf alipoteza pambano lake la 16 Bora  leo mchana mbele ya Adeiola Oyesiji wa Nigeria kwa points 5-0.
    Sasa Tanzania imebakiwa na mabondia wanne ambao bado wanaendelea kusaka nafasi za kufuzu - wengine Changalawe, Abdallah Katoto na Grace Mwakamele.
    Baada ya Dakar, yatafuatia mashindano mawili ya kidunia ya kufuzu yatakayofanyika mwakani ambapo jumla ya nafasi 100 zitagombaniwa katika michezo itakayofanyika Busto Arsizio, Italy na Bangkok, Thailand. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHANGALAWE AMTWANGA MKONGO NA KUTINGA ROBO FAINALI KUFUZU OLIMPIKI 2024 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top