• HABARI MPYA

  Saturday, September 23, 2023

  HAALAND AFUNGA MAN CITY YAICHAPA NOTTINGHAM FOREST 2-0


  MABINGWA watetezi, Manchester City wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Nottingham Forest katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Mabao ya Manchester City yamefungwa na Phil Foden dakika ya saba na Erling Haaland dakika ya 14 katika mchezo huo timu ya kocha Mspaniola, Pep Guardiola ilimaliza pungufu kufuatia Rodri kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 46 kwa kumpiga Morgan Gibbs-White wa Nottingham Forest.
  Manchester City inafikisha pointi 18 kileleni, wakati Nottingham Forest inabaki na pointi zake saba baada ya wote kucheza mechi sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HAALAND AFUNGA MAN CITY YAICHAPA NOTTINGHAM FOREST 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top