• HABARI MPYA

  Wednesday, September 20, 2023

  YANGA YAIZIMA NAMUNGO FC DAKIKA ZA MWISHONI, 1-0 CHAMAZI


  BAO la dakika ya 88 la kiungo Mzanzibari, Mudathir Yahya Abbas limeipa Yanga ushindi wa 1-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mudathir alifunga bao hilo kwa kupenyeza mguu katikati ya mlinzi Derrick Mukombozi na kipa wa Namungo FC, Deogratius Munishi ‘Dida’ kuunganishia nyavuni krosi ya winga Mkongo, Jesus Moloko.
  Mfungaji na mtoa pasi ya bao waliinuliwa kwa pamoja kutokea benchi dakika ya 67 kuchukua nafasi ya mshambuliaji mzawa, Clement Mzize na kiungo Muivory Coast, Pacome Zouazoua.
  Ushindi huo mwembamba unaifanya Yanga ifikishe pointi tisa na kurejea kileleni ikiizidi pointi mbili Mashujaa FC baada ya wote kucheza mechi tatu, wakati Namungo FC iliyocheza mechi tatu pia inabaki na pointi moja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAIZIMA NAMUNGO FC DAKIKA ZA MWISHONI, 1-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top