// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMEONE ASAINI MKATABA MPYA ATLETICO MADRID - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMEONE ASAINI MKATABA MPYA ATLETICO MADRID - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Tuesday, September 05, 2017

  SIMEONE ASAINI MKATABA MPYA ATLETICO MADRID

  KOCHA Diego Simeone amezima uwezekano wa kuhamia Inter Milan baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu kuendelea kufundisha Atletico Madrid. 
  Murgentina huyo alikuwa akihusishwa na kuhamia kwa vigogo hao wa Italia, ambao aliwachezea kuanzia mwaka 1997 hadi 1999, lakini ameamua kujifunga na waajiri wake wa sasa. 
  Simeone anapendwa mno na mashabiki wa Atletico Madrid ambao wamejenga imani kubwa kwake kufuatia kushinda taji la La Liga kama mchezaji na baadaye kocha. 
  "Kocha wetu amesaini mkataba mpya ambao unamfunga Atletico Madrid kwa misimu miwili zaidi, hadi Juni 30, mwaka 2020," imesema taarifa ya Atletico.
  Diego Simeone akirushwa juu na wachezaji wake baada ya kuiwezesha Atletico Madrid kutwaa ubingwa wa Hispania mwaka 2014 PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMEONE ASAINI MKATABA MPYA ATLETICO MADRID Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top