• HABARI MPYA

    Tuesday, September 26, 2017

    GARETH BARRY AVUNJA REKODI YA GIGGS LIGI KUU ENGLAND

    Kocha wa West Brom, Tony Pulis jana alimuanzisha Gareth Barry dhidi ya Arsenal akaweka rekodi ya kucheza mechi nyingi zaidi Ligi Kuu ya England PICHA ZAIDI GONGA HAPA  


    WALIOCHEZA MECHI NYINGI ZAIDI LIGI KUU ENGLAND KIHISTORIA 

    Gareth Barry - 633
    Ryan Giggs - 632
    Frank Lampard - 609
    David James - 572
    Gary Speed - 535
    Emile Heskey - 516
    Mark Schwarzer - 514
    Jamie Carragher - 508
    Phil Neville - 505
    Rio Ferdinand - 504
    Steven Gerrard - 504
    KIUNGO wa West Bromwich Albion, Gareth Barry jana amevunja rekodi ya nyota wa zamani wa Manchester United, Ryan Giggs kucheza mechi nyingi katika Ligi Kuu ya England.
    Barry amesema wanawe wamelazimika kutokwenda shule ili waende kumshuhudia akicheza mechi ya kuvunja rekodi usiku wa jana dhidi ya Arsenal Uwanja wa Emirates. 
    Barry, mwenye umri wa miaka 36 sasa, jana amecheza ya 633 ya Ligi Kuu England baada ya kuanzishwa kwenye mechi dhidi ya The Gunners.
    Mchezaji huyo wa zamani wa Aston Villa, Manchester City na Everton anavunja rekodi ya gwiji wa Wales, Giggs ambaye alicheza mechi 672 akiwa na Manchester United.  
    Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alimzawadia Barry jezi iliyosainiwa namba 633 na klabu hiyo ikatweet baada ya mechi: "Hongera Gareth Barry kwa kucheza mechi ta rekodi katika Ligi Kuu ya England, (pongezi) kutoka kwetu sote wa Arsenal,".
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GARETH BARRY AVUNJA REKODI YA GIGGS LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top