• HABARI MPYA

    Sunday, September 24, 2017

    WYDAD YAIVUA UBINGWA WA AFRIKA MAMELODI SUNDOWNS

    TIMU ya Wydad Casablanca ya Morocco  imeivua ubingwa wa Afrika, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini baada ya ushindi wa penalti 3-2 kufuatia sare ya jumla ya 1-1, kila timu ikishinda 1-0 nyumbani kwake Robo Fainali za Ligi ya Mabingwa.
    Wydad jana ililipa kisasi cha kufungwa 1-0 kwenye mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Uwanja wa Prince Moulay Abdallah, kabla ya kwenda kukata tiketi ya Nusu Fainali kwa ushindi wa 3-2.
    Salah Eddine Saidi aliifungia bao pekee Wydad dakika ya 11 akimalizia krosi ya Mohammed Ounajem na kufanya sare ya jumla ya 1-1 baada ya wiki iliyopita, Mamelodi pia kushinda 1-0 nchini Afrika Kusini.
    Zakri, Percy Tau, na Bangaly Soumahoro wote walikosa penaalti zao na Wydad ikashinda na kwenda Nusu Fainali, ambako watakutana na USM Alger ya Algeria.
    USM Alger imefuzu kwa mabao ya ugenini, baada ya jana kutoa sare ya 0-0 na Ferroviario Uwanja wa Julai 5, kufuatia awali kulazimisha sare ya 1-1 mjini Beira, Msumbiji.
    Nayo Al Ahly imefanikiwa kuwatoa wenyeji, Esperance de Tunis kwa ushindi wa 2-1 jana Uwanja wa Olimpiki mjini Rades, hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-3 kufuatia sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kwanza Alexandria, Misri wiki iliyopita.
    Yassine Khenissi alianza kuwafungia wenyeji jana dakika ya 40, kabla ya Ahly kutoka nyuma na kushinda kwa mabao ya Ali Maaloul dakika ya 50 na Junior Ajayi dakika ya 62.
    Etoile du Sahel wanaikaribisha Al Ahli Tripoli ya Libya Uwanja wa Olimpiki mjini Sousse, Tunisia katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya mwisho, baada ya sare ya 0-0 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Borg El Arab mjini Alxandria.
    Kikosi cha Wydad Casablanca kilikuwa: Laaroubi, Rabeh, Noussir, Atouchi, Saidi, Nakach, Gaddarine, Bencharki, Doa/El Karti dk76, Ounnajem na El Haddad/Khadrouf dk84.
    Mamelodi Sundowns: Onyango, Langerman, Arendse/Soumahoro dk89, Madisha, Mabunda, Kekana, Manyisa, Zwane/Lebese dk84, Morena, Tau na Billiat/Zakri dk73.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WYDAD YAIVUA UBINGWA WA AFRIKA MAMELODI SUNDOWNS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top