// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KIMWAGA KUFANYIWA UPASUAJI WA KUKAA NJE MIEZI MINNE AZAM FC - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KIMWAGA KUFANYIWA UPASUAJI WA KUKAA NJE MIEZI MINNE AZAM FC - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Tuesday, September 05, 2017

  KIMWAGA KUFANYIWA UPASUAJI WA KUKAA NJE MIEZI MINNE AZAM FC

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WINGA wa Azam FC, Joseph Kimwaga, anatarajia kukaa nje ya dimba kwa muda miezi minne baada ya kubainika ya kuwa amechanika mtulinga wa kati ‘meniscus’ kwenye goti lake la mguu wa kushoto.
  Kimwaga hivi sasa yupo nchini Afrika Kusini tokea Ijumaa iliyopita akifanyiwa matibabu ya goti lake hilo, aliloumia wakati Azam FC ikijiandaa na mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Ndanda ulioisha kwa matajiri hao kushinda bao 1-0 wiki mbili zilizopita.
  Daktari wa Azam FC, Mwanandi Mwankemwa, aliyeambatana na Kimwaga nchini humo, amesema kwamba mchezaji huyo alifanyiwa vipimo jana Jumatatu na Dk. Nickolas kwenye Hospitali ya Vincent Palloti iliyopo jijini Cape Town nchini humo.
  “Jumatatu (4/9/2017)alifanyiwa vipimo na kuthibitika amechanika Meniscus upande wa kati (meniscus mfano wake tunautoa kwa mafundi anapofunga nati anaweka washa kwanza halafu ndio anakaza nati juu yake Mwenyezi Mungu amemuaamba kila binadamu na hiyo washa inayoitwa meniscus, ipo katikati ya goti kuimarisha goti, ipo upande wa kati na pembeni. Hebu gusa sikio lako pembeni, meniscus inafananishwa au kulinganishwa na kuta za sikio lako).
  “Vile ameumia mtulinga wa kati ACL (Anterior Cruciate Ligament),” alisema kwenye ripoti aliyoipokea kutoka kwa Dk. Nickolas.
  Mwankemwa alisema baada ya kufanyiwa kipimo hicho, Kimwaga anatarajiwa kulazwa kesho Jumatano saa 9.00 Alasiri, huku akitarajiwa kufanyiwa upasuaji mdogo (athroscopy) siku inayofuata Alhamisi kabla ya kutoka hospitalini Septemba 9 mwaka huu na kurejea nchini siku nne baadaye (Septemba 13) saa 12.00 jioni kwenye Uwanja wa Mwl Julius Nyerere (JNIA).
  Upasuaji wa kwa njia ya Athroscopy ni ule wa kisasa kabisa ambao wataalamu hutumia vifaa maalum, ambavyo huingizwa kwenye goti ambavyo hufanya matibabu na kuondoa matatizo yote katika eneo hilo, faida yake humfanya mchezaji kurejea mapema uwanjani kuliko ule wa kupasuliwa goti zima.
  Winga huyo mara baada ya kufanyiwa upasuaji Alhamisi anatarajiwa kukaa nje ya dimba kwa kipindi cha miezi minne kutoka siku ya upasuaji.
  Azam FC tunamtakia kila kheri Kimwaga katika matibabu yake hayo, yaweze kwenda salama kama yalivyopanga na hatimaye aweze kurejea dimbani mapema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIMWAGA KUFANYIWA UPASUAJI WA KUKAA NJE MIEZI MINNE AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top