// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); CARVAJAL ASAINI MKATABA WA KUUZWA PAUNI MILIONI 308 REAL - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE CARVAJAL ASAINI MKATABA WA KUUZWA PAUNI MILIONI 308 REAL - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Monday, September 18, 2017

  CARVAJAL ASAINI MKATABA WA KUUZWA PAUNI MILIONI 308 REAL

  BEKI Dani Carvajal amesaini mkataba mpya na Real Madrid ambao ndani yake una bei ya kumuuza ambayo si rahisi mchezaji mwenyewe amesema; "Ni bei kubwa sana, hivyo kwamba hakuna yeyote anayeweza kunitoa hapa,".
  Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania ambaye ameichezea Real Madrid mechi 167, amesaini mkataba mpya leo ambao utamuweka pamoja na klabu hiyo ya La Liga hadi mwaka 2022.
  Kufuatia kuondoka kwa Neymar kwa dau la Pauni Milioni 198 kwenda Paris Saint-Germain msimu huu, mkataba wa Carvajal unahusisha na kipengele cha kuuzwa kwa Pauni Milioni 308 - bei ambayo beki huyo anatumai itamuhakikishia kudumu hadi mwisho wa mkataba wake katika klabu hiyo.
  Dani Carvajal akipewa jezi namba 2022 kuashiria kusaini mkataba ambao utamalkizika mwaka 2022 Real Madrid PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  "Klabu hii ni sehemu kubwa ya maisha yangu, hivyo kwangu huku ni kukamilika kwa ndoto zangu,"amesema baada ya kuongeza muda wake wa kuendelea kufanya kazi Bernabeu.
  Carvajal aliibukia katika akademi ya vijana ya Real Madrid kabla ya kuhamia Bayer Leverkusen ya Ujerumani mwaka 2012. 
  Alirejea katika klabu yake ya utotoni mwaka mmoja baadaye na tangu hapo amekuwa mmoja wa mabeki bora wa kulia duniani.
  Na amesema anafikiria simu moja kurithi kitambaa cha Unahodha wa klabu kutoka kwa Nahodha wa sasa, Sergio Ramos. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CARVAJAL ASAINI MKATABA WA KUUZWA PAUNI MILIONI 308 REAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top