• HABARI MPYA

  Tuesday, September 26, 2017

  MRUNDI KUMRITHI PHIRI MBEYA CITY, APEWA MKATABA WA MWAKA MMOJA

  Na Mwandishi Wetu, MBEYA
  MRUNDI Nsanzurwino Ramadhani ndiye Kocha Mkuu mpya wa Mbeya City FC anayechukua nafasi ya Mmalawi, Kinnah Phiri aliyeondoka rasmi mwezi huu.
  Taarifa ya Mbeya City Jumatatu usiku imesema kwamba Nsanzurwino Ramadhani anakuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo kwa mkataba wa awali wa msimu mmoja wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inayoendelea.
  “Kocha Ramadhan ni raia wa Burundi na anatarajia kujiunga na timu huko kanda ya ziwa inakoendelea na michezo ya Ligi Kuu. Ramadhani amewahi kuwa kocha kwa nyakati tofauti katika klabu mbalimbali nchini Burundi, Rwanda, Botswana, Malawi, Uganda na Afrika Kusini,”imesema taarifa ya MCC.
  Nsanzurwino Ramadhani ndiye Kocha Mkuu mpya wa Mbeya City FC anayechukua nafasi ya Mmalawi, Kinnah Phiri aliyeondoka rasmi mwezi huu

  Mrundi huyo pia amewahi kuwa Mshauri wa Ufundi katika timu ya taifa ya nchi yake, Burundi na kocha Msaidizi, Kocha Mkuu wa Muda wa timu ya taifa ya Malawi. 
  Ramadhani atakuwa kocha wa tatu wa Mbeya City tangu ipande Ligi Kuu misimu minne iliyopita, baada ya Juma Mwambusi aliyeipandisha na Phiri na kama watangulizi wake, naye ataendelea kusaidiwa na mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Mohammed Kijuso.
  Kijuso ambaye pia ni mshambuliaji wa zamani wa Simba, amekuwa kaimu kocha mkuu tangu mwanzo wa msimu huu kufuatia kuondoka kwa Phiri.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MRUNDI KUMRITHI PHIRI MBEYA CITY, APEWA MKATABA WA MWAKA MMOJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top