• HABARI MPYA

  Friday, September 29, 2017

  CECAFA CHALLENGE YARUDI, KUFANYIKA KENYA 2017

  BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limeitaja Kenya kuwa mwenyeji wa Kombe la mataifa ya ukanda huo, maarufu kama Senior Challenge Cup mwaka huu.
  CECAFA inatangaza kufanyika tena kwa Challenge mwaka huu, ikiwa ni miaka miwili tangu ilipofanyika kwa mara ya mwisho nchini Ethiopia.
  Katika Mkutano wake wa Kamati ya Utendaji uliofanyika mjini Khartoum, Sudan, Wajumbe walikubaliana kuungana na Kenya baada ya kushindwa kuwa mwenyeji wa Fainali za tano za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) zinazohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pejee Januari mwaka 2018.
  Michuano ya CECAFA Challenge Cup, ambayo inazikutanisha timu zote za nchi 13 wanachama wake, witafanyika kati ya Novemba na Desemba 2017.
  Uganda ndio mabingwa wa sasa wakiwa pia wanashikilia rekodi ya kutwaa mara nyingi taji hilo, mara 14 kufuatia kulibeba pia na mjini Addis Ababa Desemba 2015 baada ya kuifunga Rwanda 1-0 kwenye fainali.
  Kikao pia kiliamua Burundi na Rwanda wawe wenyeji wa michuano ya vijana ya Cecafa chini ya umri wa miaka 17 na wanawake ambayo pia itafanyika Novemba na Desemba.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CECAFA CHALLENGE YARUDI, KUFANYIKA KENYA 2017 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top