// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MAMELODI YABISHA HODI NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MAMELODI YABISHA HODI NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Monday, September 18, 2017

  MAMELODI YABISHA HODI NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA

  TIMU ya Mamelodi Sundowns jana imepata ushindi mwembamba wa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Athletic Club ya Morocco Uwanja wa Lucas Moripe.
  Bao pekee la mabingwa hao watetezi jana lilifungwa na Krahire Zakri dakika ya 71 na sasa Mamelodi inakuwa timu pekee iliyoshinda robo fainali ya kwanza msimu huu baada ya nyingine zote kutoa sare.
  Lakini Mamelodi watakuwa na kibarua kigumu kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Wydad mjini Cassablanca kuhakikisha wanakwenda kulazimisha sare ili kusonga mbele.
  Mchezo mwingine wa jana, Al Ahli Tripoli ya Libya ililazimishwa sare ya 0-0 na Etoile du Sahel ya Tunisia Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria.
  Juzi zilichezwa mechi mbili ambazo zote zilimalizika kwa sare pia, Al Ahly SC wakifungana 2-2 na Esperance Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria na Ferroviario Beira wakitoka 1-1 na USM Alger ya Algeria Uwanja wa Ferroviario mjini Beira.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAMELODI YABISHA HODI NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top