• HABARI MPYA

  Friday, September 29, 2017

  AGUERO AVUNJIKA MBAVU KWENYE AJALI YA GARI UHOLANZI

  MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Sergio Aguero ameripotiwa kuvunjika mbavu ya nyota huyo wa Argentina kupata ajali mjini Amsterdam usiku wa Alhamisi.
  Gazeti la Diairio Ole la Argentina limesema kwamba Aguero, ambaye alikuwa Uholanzi kuhudhuria tamasha la mwimbaji wa Colombia, Maluma, alikuwa kwenye teksi wakati anapata ajali.
  Aguero, mwenye umri wa miaka 29, imeelezwa hajapata majeraha zaidi kwa sababu alikuwa amejifunga mkanda wa kiti wakati ajali inatokea kwa teksi kuacha barabara na kwenda kugonga nguzo pembeni.
  Imeelezwa ajali hiyo ilitokea wakati mchezaji huyo anakwenda Uwanja wa Ndege, lakini inafikiriwa alikwenda kupatiwa matibabu baada ya ajali hiyo.
  Hii ndiyo gari aliyokuwamo Sergio Aguero baada ya kuacha barabara na kwenda kugonga nguzo pembeni 

  Taarifa nchini Argentina zinasema mchezaji huyo anaweza kuwa nje kwa miezi hadi miwili kutokana na maumivu hayo, kufuatia ajali hiyo iliyohusisha gari aina ya Chrysler PT Cruiser aliyokuwamo. 
  Mapema Alhamisi jioni, Aguero aliposti picha kwenye ukurasa wake Instagram akiwa na Maluma, akimshukuru nyota huyo wa Colombia kwa kumpa mwaliko wa kwenye tamasha hilo, lililofanyika ukumbi wa AFAS Live, jirani na Uwanja wa Ajax wa Amsterdam Arena. 
  Maluma pia aliposti picha ya Aguero akimsainia jezi ya Manchester City, akiambatanisha na maelezo 'Urafiki na mpira vidumu, asante kwa maandishi,"'. 
  City haijasema chochote juu ya taarifa hizo, lakini klabu yake ya zamani nchini Argentina, Independiente, imesema kwenye Twitter: "Imarika na upone haraka. Independiente wote wapo nawe katika wakati huu mgumu,".
  Vinara wa Ligi Kuu ya England, Man City watamenyana na Chelsea Uwanja wa Stamford Bridge Jumamosi.
  Aguero amekuwa katika kiwango kizuri msimu huu kama kawaida, akifunga mabao saba kwenye mashindano yote hadi sasa na kubakiza goli moja tu kufikia rekodi ya Eric Brook ya ufungaji bora wa muda wote wa City.
  Kuumia kwake ni pigo kwa City ambayo tayari inamkosa beki wa kushoto, Benjamin Mendy, ambaye anatarajiwa kuikosa sehemu iliyobaki ya msimu kutokana na kuwa majeruhi. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AGUERO AVUNJIKA MBAVU KWENYE AJALI YA GARI UHOLANZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top