• HABARI MPYA

  Wednesday, September 20, 2017

  BENZEMA KUSAINI MKATABA REAL MADRID ATAUZWA EURO BILIONI 1

  KLABU ya Real Madrid imekubali kusaini mkataba mpya na Karim Benzema aendelee kufanya kazi Uwanja wa Bernabeu hadi mwaka 2021.
  Benzema, ambaye amewafungia mabao zaidi ya 170 mabingwa hao wa Hispania tangu ajiunge nao mwaka 2009 kutoka Lyon ya kwao, Ufaransa, atasaini mkataba mpya ambao imeripotiwa atakuwa analipwa Euro Milioni 7.5 kwa mwaka
  Kwa mujibu wa taarifa nchini Hispania, mkataba wa mshambuliaji huyo una kipengele cha kuuzwa kwa Euro Bilioni 1 timu ikimhitaji. 
  Karim Benzema atasaini mkataba mpya Real Madrid utakaomuweka Santiago Bernabeu hadi mwaka 2021 PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2019, lakini Benzema atafuata nyayo za Isco na Dani Carvajal kujifunga kuendelea kuichezea timu hiyo.
  Katika taarifa ya klabu iliyotolewa leo, Real Madrid imesema Mfaransa huyo atasaini mkataba huo mbele ya vyombo vya Habari Alhamsi mchana.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, ambaye ameshinda mataji 14 katika kipindi chote cha kuwa Real, sasa atabaki na Los Blancos hadi atakjapotimiza miaka 33.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BENZEMA KUSAINI MKATABA REAL MADRID ATAUZWA EURO BILIONI 1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top