• HABARI MPYA

  Tuesday, September 19, 2017

  KIPA MGHANA WA AZAM HATAKI KUFUNGWA LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIPA namba moja wa Azam FC, Mghana, Razack Abalora amesema anataka kuendeleza rekodi yake ya kudaka bila kufungwa katika mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online jana, Abalora aliyedaka mechi tatu za awali za Ligi Kuu bila kuruhusu nyavu zake kuguswa, amesema kwamba anataka kuendeleza rekodi hiyo nzuri.
  “Kila kipa lengo lake ni kudaka bila kufungwa katika klabu yake, nami nina furaha kudaka mechi tatu za Ligi Kuu bila kufungwa Azam FC, lengo lengo ni kuendelea kudaka bila kufungwa ili niisaidie timu yangu kushinda,”amesema.
  Razack Abalora anataka kuendeleza rekodi yake nzuri katika Ligi Kuu
  Abalora alisimama langoni Azam FC ikishinda 1-0 mara mbili, kwanza ugenini dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona na baadaye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam dhidi ya Kagera Sugar, wakitoka kutoa sare ya 0-0 na Simba.   
  Kikosi chaAzam FC kinatarajiwa kushuka tena dimbani hapo hapo Azam Complex, kumenyana na Lipuli ya Iringa Jumapili wiki hii kuanzia Saa 1.00 usiku na kwa sasa kipo kwenye mazoezi makali kujiandaa na mchezo huo.
  Mbali na mazoezi ya uwanjani, benchi la ufundi la timu hiyo chini ya Aristica Cioaba, limekuwa na utaratibu wa kuwajenga wachezaji kimwili kwa kufanya programu maalum ya gym kila wiki mara moja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIPA MGHANA WA AZAM HATAKI KUFUNGWA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top