• HABARI MPYA

    Saturday, September 30, 2017

    HAKUNA MBABE USM ALGER NA WYDAD, WATOKA SULUHU

    WENYEJI, USM Alger wamelazimishwa sare ya 0-0 na Wydad Casablanca ya Morocco katika Nusu Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika usiku wa jana Uwanja wa Julai 5 mjini Algiers.
    Timu hizo zilishambuliana kwa zamu katika mchezo na kosakosa zilikuwa za pande zote. 
    Kwa matokeo hayo, mchezo wa marudiano Oktoba 20 mjini Casablanca nchini Morocco ndio utaamua timu ya kwenda Fainali.
    Mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla ya mechi kati ya Al Ahly ya Misri na Etoile du Sahel ya tunisia.
    Katika hatua nyingine, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limesogeza mbele kwa siku moja Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho baina ya SuperSport United ya Afrika Kusini na Club Africain ya Tunisia kutoka Jumamosi hadi Jumapili.
    Mchezo huo sasa utafanyika Uwanja wa Lucas 'Masterpieces' Moripe mjini Pretoria Jumapili ya Oktoba 1 kutokana na sababu za kiufundi, zilizosababisha msafara wa wageni kutuoka Tunisia uchelewe kufika Afrika Kusini.
    Wakitoka kuitoa Zesco United ya Zambia kwa mabao ya ugenini, SuperSport wana matumaini ya kuendeleza rekodi yao nzuri.
    Walianza kwa sare ya 0-0 nyumabi, kabla ya kwenda kutoa sare ya 2-2 na Timh ya Ziko ugenini ambako kiungo, Thuso Phala alifunga mabao mawili mjini Ndola na anatarajiwa kuiongzoa timu yake tena dhidi ya Watunisia.
    Nusu Fainali nyingine ya michuano hiyo itazikutanisha TP Mazembe ya DRC na FUS Rabat ya Morocco Uwanja wa TP Mazembe mjini Lubumbashi Jumapili pia, wakati timu zote zitarudiana Oktoba 20, mwaka huu kusaka timu za kucheza fainali ya 2017.
    Mechi za jana vikosi vilikuwa, Alger: Zemmamouche, Meftah, Chafai, Abdellaoui, Benmoussa, Benguit, Benkhemassa, Meziane/Benkablia dk84, Hamzaoui/Hammar dk68, Sayoud na Darfalou.
    Wydad: Laaroubi, Rabeh, Noussir, Atouchi, Saidi, El Karti/Khadrouf dk88, Nakach, Gaddarine, Bencharki, Doa/El Haddad dk72 na Ounajem.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HAKUNA MBABE USM ALGER NA WYDAD, WATOKA SULUHU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top