• HABARI MPYA

  Wednesday, September 20, 2017

  SANGA AUNDA KAMATI SABA ‘NZITO’ YANGA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAIMU Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga ameunda Kamati Saba za kushughulikia masuala mbalimbali ya klabu hiyo.
  Taarifa ya Yanga kwa vyombo vya Habari jioni ya leo, imezitaja Kamati hizo ni ya Fedha Uchumi na Mipango, Uwanja na Jengo, Sheria, Jengo la Mafia, Masoko na Wanachaama, Ufundi na ya Soka la Vijana.
  Katika Kamati ya Fedha Uchumi na Mipango, Sanga amemteua Mohammed Nyenge kuwa Mwenyekiti na Wajumbe Baraka Deusdedit, Lawrence Mafuru, Erald Mutalemwa, Ivan Tarimo, Abuu Faraj na Anthony Mark.
  Clement Sanga (kushoto) amemteua kocha George Lwandamina kwenye Kaamti ya Ufundi
  Katika Kamati ya Uwanja wa Kaunda na Jengo la makao makuu, Jangwani, Dar es Salaam, Sanga mwenyewe atakuwa Mwenyekiti pamoja na Wajumbe, Charles Boniface Mkwasa, Omary Said, Milton Nyerere, Deo Steven, Iddi Salum Mohammed, Aidan Haule, Nassor Duduma, Shaaaban Mwatawala, Mohammed Chambo, Bakiri Makere, Robert Kasela, David Luhago na Mohammed Nassor.
  Kamati ya Sheria itakuwa chini ya Mwenyekiti Jaji Anthony Mark, Onesmo Mpinzile, Teddy Kalua, Peter Hella, Gaudioson Ishengoma na Mustapha Kambona, wakati Kamati ya Jengo la Mafia itaongozwa na Mwenyekiti, Thobias Lingalangala, Inspekta Hashim Abdallah, Siza Lyimo, Lucas Kisasa, Genera Kiwamba na Madaraka Malumbo.
  Kamati ya Masoko na Wanachaama itakuwa chini ya Mwenyekiti, Salum Mkemi, Samuel Lukumay, Omar Kaaya, Aaron Nyanda, Ray Kigosi, Abeid mziba na Hajji Mboto, wakati Kamati ya Ufundi itakuwa chini ya mwenyewe Sanga kama Mwenyekiti na Wajumbe Charles Boniface, Kocha Mkuu wa timu, Mzambia George Lwandamina, Mustapha Ulungo, Hussein Nyika, Keneth Mkapa na Ally Mayay Tembele.
  Katika Kamati ya Soka la Vijana, Mwenyekiti atakuwa Ayoub Nyenzi na Wajumbe Islam Hamad, Said Maulid ‘SMG’, Edibily Lunyamila, Omary Kapilima, Mohammed Hussein ‘Mmachinga’, Ramadhani Kampira na Omar Kaaya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SANGA AUNDA KAMATI SABA ‘NZITO’ YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top