• HABARI MPYA

    Monday, September 25, 2017

    AZAM FC YAIKAMATA MTIBWA SUGAR KILELENI LIGI KUU

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU ya Azam FC, imeendelea kufanya kweli kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuichapa Lipuli bao 1-0, mchezo uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam usiku wa Jumapili.
    Kwa ushindi huo Azam FC imefanikiwa kuikamata Mtibwa Sugar baada ya kufikisha jumla ya pointi 10 zikiwa zinalingana kileleni huku ikiwa timu pekee ambayo haijaruhusu bao lolote tokea ligi hiyo ilipoanza Agosti 26 mwaka huu.
    Bao pekee la Azam FC limefungwa na Mbaraka Yussuf dakika ya 11 akipokea pasi safi ya Nahodha Himid Mao ‘Ninja’, likiwa ni bao lake la pili kwenye mechi ya pili mfululizo lingine akiitungua timu yake ya zamani Kagera Sugar katika ushindi wa 1-0.
    Mbaraka Yussuf akikimbia kushangilia baada ya kuifungia Azam FC bao pekee leo

    Licha ya kufunga bao hilo, Azam FC ilifanikiwa kutawala mchezo huo kwa kiasi kikubwa na kutengeneza nafasi nyingi takribani 10 ambazo hazikutumiwa vema.
    Lakini safu ya ushambuliaji ilikuwa ikiundwa na wachezaji vijana Yahya Zayd na Yusuph, ambao wanaendelea kujifunza mikikimikiki ya ligi hiyo,
    Kabla ya mchezo huo, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, alipata fursa ya kuwakabishi tuzo za wachezaji bora wa Azam FC mwezi Agosti, beki Yakubu Mohammed, akitwaa kwa upande wa timu kubwa na kiungo Twaha Ahmed, akibeba ya timu ndogo (Azam B).
    Mara baada ya mchezo huo, kikosi cha Azam FC kinatarajia kupumzika kesho Jumatatu kanla ya kuanza mazoezi Jumanne kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Singida United, uutakaofanyika Uwanja wa Jamhuri Dodoma Septemba 30 mwaka huu.
    Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Razak Abalora, Himid Mao, Bruce Kangwa, Aggrey Morris, Yakubu Mohammed, Daniel Amoah, Stephan Kingue/Braison Raphael dk59, Frank Domayo, Salum Abubakar, Yahya Zayd/Waziri Junior dk59, Mbaraka Yusuph/Yahaya Mohammed dk79
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAIKAMATA MTIBWA SUGAR KILELENI LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top