• HABARI MPYA

  Monday, September 25, 2017

  TP MAZEMBE YAENDA NUSU FAINALI KWA KISHINDO

  TIMU ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) jana imeibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Al-Hilal Al-Ubayyid katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa TP Mazembe mjini Lubumbashi.
  Mabao ya Mazembe jana yalifungwa na Jean Kasasula dakika ya 39, Adama Traore dakika ya 49, Malango Ngita dakika ya 55, Elia Meshack dakika ya 84 na Djos Issama dakika ya 90 na ushei na kwa matokeo hayo, timu hiyo ya Lubumbashi inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 7-1, baada ya kushinda ugenini pia wiki iliyopita 2-1.
  Mabingwa hao wa zamani wa Afrika, sasa watakutana na FUS Rabat ya Morocco katika Nusu Fainali.
  Nayo Club African ya Tunisia imefanikiwa pia kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya MC Alger 2-0 usiku wa jana Uwanja wa Olimpiki mjini Rades.
  Ushindi huo, unamaanisha MC Alger inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 2-1 baada ya awali kufungwa 1-0 na Waalgeria hao kwenye mchezo wa kwanza.
  Mabao ya Club Africain jana yalifungwa na Moataz Zemizemi kwa penalti na mkongwe, Saber Khalifa na sasa watakutana na SuperSport United ya Afrika Kusini ambayo imeitoa ZESCOUnited ya Zambia kwa mabao ya ugenini kufuatia sare ya 2-2 Uwanja wa Levy Mwanawasa mjini Ndola juzi baada ya sare ya 0-0 kwenye mchezo wa kwanza Septemba 15.
  Kikosi cha Mazembe kilikuwa; TP Mazembe: Gbohouo, Kasusula, Issama, Chongo, Mondeko, Sinkala, Nii/Koffi dk77, Kalaba/Meshack dk81, Traore, Malango, Ushindi/Asante dk71.
  Al-Hilal: Salim, Ishag/Girfa dk48, Bachir, Alkhidir, Amin, Hassan, Shighail, Ladzagla, Musa/Kiza dk51, Hassan, Maaz na Gismalla/Tahir dk62.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TP MAZEMBE YAENDA NUSU FAINALI KWA KISHINDO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top