• HABARI MPYA

  Tuesday, September 26, 2017

  KICHUYA AANZA MAZOEZI CHINI YA UANGALIZI WA DAKTARI MWANZA

  Na Mwandishi Wetu, MWANZA
  WINGA tegemeo wa Simba, Shiza Ramadhani Kichuya leo ameanza mazoezi na timu yake baada ya kupata ahueni ya maumivu ya kifundo cha mguu.
  Kichuya aliumia dakika ya 44 katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania dhidi ya wenyeji, Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza na nafasi yake kuchukuliwa na Haruna Niyonzima.
  Na Kichuya aliondoka uwanjani akiwa tayari amekwishaifungia Simba bao la kuongoza katika mchezo ambao mwishowe ulimalizika kwa sare ya 2-2.
  Shiza Kichuya (kulia) leo ameanza mazoezi chini ya uangalizi wa Daktari mjini Mwanza

  Shiza Kichuya aliondoka uwanjani akiwa tayari amekwishaifungia Simba bao la kuongoza katika mchezo ambao mwishowe ulimalizika kwa sare ya 2-2


  Winga huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar ya Morogoro akaenda kukosa mchezo wa kirafiki dhidi ya Milambo FC juzi Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, timu hizo zikitoka sare ya 0-0.
  Lakini leo asubuhi Kichuya amefanya mazoezi chini ya usimamizi wa Daktari wa timu hiyo, Yassin Gembe Uwanja wa Alliance mjini Mwanza.
  Simba imerejea Mwanza jana kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo wake ujao wa Ligi Kuu dhidi ya wenyeji, Stand United United Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga Oktoba 1, mwaka huu. 
  Tayari Simba SC imekwishacheza mechi nne za Ligi Kuu, ikishinda mbili 7-0 dhidi ya Ruvu na 3-0 dhidi ya Mwadui FC zote Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam wakati nyingine mbili imetoa sare ugenini 0-0 na Azam FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi na 2-2 na Mbao FC Mwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KICHUYA AANZA MAZOEZI CHINI YA UANGALIZI WA DAKTARI MWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top