• HABARI MPYA

    Saturday, June 13, 2026

    SUNDAY KAYUNI ATEULIWA KUWA MKURUGENZI WA UFUNDI ZAMBIA


    SHIRIKISHO la Soka Zambia limemteua Mtanzania Sunday Burton Kayuni (70) kuwa Mkurugenzi wake mpya wa Ufundi akichukua nafasi ya mzawa, Lyson Zulu aliyedumu tangu Machi 2019.
    Zulu aliondoka FAZ mapema mwaka huu baada ya kuteuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kuwa Mtaalamu wa Utendaji Bora wa Mpango wa Maendeleo ya Kiufundi (TDS) kwa Afrika Januari mwaka huu.
    Kayuni (pichani kulia) ambaye ni Mkufunzi Mkubwa wa FIFA - ni Mtaalamu mwenye heshima kubwa Zambia na Afrika kwa ujumla kutokana na 
    Uzoefu wake na rekodi ya kuvutia ya kuwafundisha makocha kadhaa wa Zambia, akiwemo George Lwandamina, ambaye kwa sasa anaiongoza timu ya taifa.
    Licha ya kufundisha klabu mbalimbali Tanzania na kwa mafanikio wakiwemo mabingwa wa kihistoria nchini na timu ya taifa – Kayuni pia amewahi kuwa Mkurugenzi wa Ufundi na Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SUNDAY KAYUNI ATEULIWA KUWA MKURUGENZI WA UFUNDI ZAMBIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top