• HABARI MPYA

  Tuesday, September 26, 2017

  LACAZETTE AANGUKIA KWENYE VIPIMO BAADA YA KUFUNGA MAWILI JANA

  KUFUATIA kufunga mabao yote mawili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya West Brom kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa Emirates, mshambuliaji Alexandre Lacazette jana alipimwa kama anatumia dawa za kuongeza nguvu zilizopigwa marufuku michezoni.
  Hiyo ni katika utaratibu wa kawaida mchezaji wa yeyote huteuliwa baada ya mechi kwa ajili ya vipimo hivyo na jana uteuzi ulimuangukia Mfaransa huyo.
  Naye baada ya kufanyiwa vipimo hivyo akaenda kuposti kwa utani kwenye akaunti yake Twitter kwamba alipimwa kutokana na kucheza vizuri jana na kufunga mabao hayo mawili.  

  Alexandre Lacazette ametania kwamba amefanyiwa vipimo kwa sababu ya kufunga mabao mawili jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Mshambuliaji huyo ameposti picha yake baada ya mchezo ikiwa imeambatana na maelezo: "Mabao mawili.. unapelekwa kwenye vipimo?? Mmefanya vizuri vijana.'
  Mshambuliaji huyo anaweza kuwa hajavutiwa na kufanyiwa vipimo hivyo, lakini kocha wake alivutiwa kupita kiasi kwa kazi yake nzuri kwenye mchezo huo.
  Akizungumza baada ya mchezo huo kwa furaha ya timu yake kubeba pointi tatu, Arsene Wenger alisema: "Naamini kwamba anaimarika katika kila mchezo. Ni kijana na ndiyo anawasili England. Mahitaji ya nguvu ni makubwa mno",.
  "Kiufundi yuko vizuri na unaweza kumuona kwenye mipira ya adhabu, anakuwa ananyemelea mipira inayorudi kama washmbuliaji wengine wote wazuri.'
  Pointi hizo tatu zinaipandisha Arsenal hadi nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England, kuelekea kwenye mchezo wake wa Europa League dhidi ya BATE Borisov Alhamisi.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LACAZETTE AANGUKIA KWENYE VIPIMO BAADA YA KUFUNGA MAWILI JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top