// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA KUENDELEA KUMKOSA TAMBWE KESHO MECHI NA NDANDA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA KUENDELEA KUMKOSA TAMBWE KESHO MECHI NA NDANDA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Friday, September 22, 2017

  YANGA KUENDELEA KUMKOSA TAMBWE KESHO MECHI NA NDANDA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  YANGA SC itaendelea kumkosa mshambuliaji wake tegemeo, Mrundi Amissi Tambwe katika mchezo wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ndanda FC kesho Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
  Kocha Msaidizi wa Yanga, Nsajigwa Shadrack amesema leo katika mkutano na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam kwamba Tambwe ndiye mchezaji pekee ambaye ataendelea kukosekana kesho.
  Amesema wachezaji wengine wote wapo fiti kuelekea mchezo huo wa nne wa Ligi Kuu, timu ikitoka kushinda mechi moja tu na kutoa sare mbili. “Kwa ujumla kikosi chetu kipo vizuri kabisa kuelekea mchezo wa kesho,”amesema Nsajigwa.
  Yanga itaendelea kumkosa Amissi Tambwe katika mchezo wa kesho dhidi ya Ndanda FC 

  Kiungo Thabani Kamusoko aliyeukosa mchezo uliopita dhidi ya Maji Maji mjini Songea, Yanga ikilazimishwa sare ya 1-1 atakuwepo pamoja na mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa aliyecheza mechi mbili zilizopita akitoka kwua nje kwa muda mrefu sababu ya maumivu ya goti.
  Tambwe amekuwa nje tangu mwanzoni mwa msimu kutokana na maumivu ya goti, ambayo yalimuanza msimu uliopita na sasa yanaelekea kuwa sugu. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA KUENDELEA KUMKOSA TAMBWE KESHO MECHI NA NDANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top