• HABARI MPYA

    Sunday, June 14, 2026

    MPANZU NA LIBASSE GUEYE WAFUNGA SIMBA SC YAICHAPA PAMBA JIJI 2-1 MWENGE


    VIGOGO, Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Pamba Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
    Mabao ya Simba SC yote yamefungwa na mawinga wa kigeni, Mkongo Elie Mpanzu Kibisawala dakika ya na nane Msenegal, Libasse Gueye dakika ya 65, huku bao pekee la Pamba Jiji FC likifungwa na mshambuliaji wake Mkenya, Mathew Tegisi Momanyi dakika ya 18.
    Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 61, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili na mabingwa watetezi, Yanga SC baada ya timu hizo zote kucheza mechi 26. 
    Nayo Pamba Jiji FC kwa upande wake pamoja na kupoteza mchezo huo inabaki nafasi ya saba ikiwa na pointi 33 ikiizidi tu wastani wa mabao Dodoma Jiji FC baada ya timu hizo nao zote kuchea mechi 26. 
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja, wakati nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.    

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MPANZU NA LIBASSE GUEYE WAFUNGA SIMBA SC YAICHAPA PAMBA JIJI 2-1 MWENGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top