// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AZAM FC YAWACHOMOLEA SINGIDA UNITED DAKIKA ZA MWISHONI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AZAM FC YAWACHOMOLEA SINGIDA UNITED DAKIKA ZA MWISHONI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Saturday, September 30, 2017

  AZAM FC YAWACHOMOLEA SINGIDA UNITED DAKIKA ZA MWISHONI

  Na Mwandishi Wetu, DODOMA
  TIMU ya Azam FC imelazimisha sare ya 1-1 na wenyeji wahamiaji, Singida United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
  Kwa matokeo hayo, Azam FC inafikisha pointi 11 baada ya kucheza mechi tano, ikishinda tatu na kutoa sare ya pili leo, wakati Singida United inafikisha pointi 10 leo, kutokana na kushinda mechi tatu, kufungwa moja na kutoa sare moja.
  Katika mchezo wa leo, Singida United walitangulia kwa bao la mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda, Danny Usengimana dakika ya 39, kabla ya Peter Paul aliyetokea benchi kuisawazishia Azam FC dakika ya 87.
  Chipukizi Peter Paul (kulia) akikimbia na wenzake kushangilia baada ya kuifungia Azam FC bao la kusawazishia mwishoni mwa mchezo


  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Mwadui FC wametoka sare ya 2-2 na Mbeya City Uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga, Mbao FC wametoka sare ya 1-1 na Tanzania Prisons Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza na Maji Maji wametoka sare ya 0-0 na Kagera Sugar Uwanja wa Maji Maji mjini Songea.
  Ruvu Shooting nao wametoa sare ya pili mfululizo nyumbani, wakitoka 1-1 na Njombe FC Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani, wakati Ndanda FC wao ndiyo pekee wameweza kuibuka na ushindi leo, baada ya kuichapa 2-1 ya Iringa Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAWACHOMOLEA SINGIDA UNITED DAKIKA ZA MWISHONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top