• HABARI MPYA

    Friday, September 22, 2017

    KICHUYA ANAENDELEA VIZURI SIMBA SC

    Na Rehema Liucas, MWANZA
    WINGA wa Simba SC, Shiza Ramadhani Kichuya anaendelea vizuri chini ya uangalizi wa madaktari baada ya jana kuumia kipindi cha kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
    Katika mchezo huo uliomalizika kwa sare ya 2-2, Kichuya aliondoka uwanjani anachechemea dakika ya 44 baada ya kuumia kifundo cha mguu akitoka kuifungia Simba SC bao la kuongoza dakika ya 16, nafasi yake ikichukuliwa na kiungo kutoka Rwanda, Haruna Niyonzima. 
    Daktari wa Simba SC, Yassin Gembe amesema leo mjini Mwana kwamba kijana huyo anaendelea na matibabu na yuko chini ya uangalizi mzuri wa matabibu wa timu. 
    Shiza Kichuya akipatiwa matibabu jana Uwanja wa CCM Kirumba baada ya kuumia kifundo cha mguu kipindi cha kwanza 

    Simba jana ililazimisha sare ya 2-2 na Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, hiyp ikiwa sare ya pili kwa Simba ndani ya mechi nne, kufuatia awali kulazimishwa sare ya 0-0 na Azam FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Mechi nyingine, Simba imeshinda 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting na 3-0 dhidi ya Mwadui FC zote Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.   
    Katika mchezo wa leo uliochezeshwa na refa Athumani Lazi wa Morogoro, hadi mapumziko Simba walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililofungwa na winga machachari, Shiza Ramadhani Kichuya dakika ya 16 akimalizia krosi nzuri ya beki Erasto Edward Nyoni.
    Kipindi cha pili Mbao walirudi kwa kasi nzuri na kufanikiwa kusawazisha bao dakika ya 46 tu, kupitia kw3a Habib Kiyombo ambaye hilo linakuwa bao lake la tatu msimu huu.
    Hata hivyo, Simba walijibu kwa mashambulizi mfululizo na kufanikiwa kupata bao la pili dakika tatu baadaye, mfungaji kiungo Mghana, James Kotei.   
    Mbao hawakukata tamaa, waliendelea kushambulia na kufanikiwa kusawazisha tena dakika ya 81 kupitia Boniphace Maganga aliyefunga kwa shuti la mbali pia.
    Simba SC itashuka tena dimbani Oktoba 1, kumenyana na wenyeji, Stand United Uwanja wa Kambarage, Shinyanga. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KICHUYA ANAENDELEA VIZURI SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top