• HABARI MPYA

  Monday, September 25, 2017

  OZIL NA SANCHEZ WOTE FITI ARSENAL IKIIVAA WEST BROM LEO

  NYOTA Jack Wilshere, Mesut Ozil na Alexis Sanchez ni miongoni mwa wachezaji wa Arsenal waliofanya mazoezi jana kuelekea mchezo wa Ligi Kuu ya England leo dbhidi ya West Brom.
  Kikosi cha Arsene Wenger kinawakaribisha The Baggies Uwanja wa Emirates usiku wa Jumatatu ya leo kikiwa na matumaini ya kuendeleza rekodi yao nzuri ya nyumbani msimu huu.
  Arsenal tayari imezifunga Leicester City, AFC Bournemouth, Doncaster na Cologne Uwanja wa Emirates msimu huu, wakati West Brom haijashinda ugenini kwenye ligi tangu wiki ya pili ya msimu.

  Arsene Wenger (kulia) akiwa na mshambuliaji wake tegemeo, Alexis Sanchez aliyechuchumaa kushoto mazoezini jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA


  Kikosi cha Pulis kina rekodi yake aina yake mbele ya Arsenal, kikiwa kimeshinda mechi moja tu kati ya 14 walizosafiri kwenda Kaskazini mwa London.
  Kwa sasa The Baggies wanajivunia mchezaji ambaye ambaye anawajua vizuri The Gunners, Kieran Gibbs ambaye ameondoka Arsenal kuhamia The Hawthorns msimu huu kwa ada ya Pauni Milioni 7. 
  Beki huyo wa kushoto aliyejiunga na akademi ya Arsenal akiwa ana umri wa miaka 10, amecheza jumla ya mechi 230 The Gunners na Wenger alikiri kuumia baada ya mchezaji huyo kuondoka akikimbia benchi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OZIL NA SANCHEZ WOTE FITI ARSENAL IKIIVAA WEST BROM LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top