• HABARI MPYA

    Saturday, September 23, 2017

    AZAM FC YAJIVUNIA REKODI YA KUTOFUNGIKA LIGI KUU

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU ya Azam FC ndiyo pekee ambayo haijaruhusu nyavu zake kuguswa katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara iliyanza Agosti 26, mwaka huu.
    Azam FC imefanikiwa kukamilisha dakika 270 bila ya nyavu zake kuguswa, kutokana na umahiri wak kipa wake, Mghana, Razak Abalora aliyepachikwa jina la utani ‘mikono 100’ na mashabiki wa timu hiyo.
    Pamoja na umahiri wake langoni, lakini Abalora anajivunia safu imara ya ulinzi inayomlinda, ambayo inaundwa na mabeki Waghana wenzake, Yakubu Mohammed, Daniel Amoah, Mzimbabwe, Bruce Kangwa na Mzanzibari, Aggrey Morris.
    Kipa Mghana wa Azam, Razak Abalora (kulia) amepachikwa jina la utani ‘mikono 100’ na mashabiki wa timu hiyo

    Mabingwa hao wa zamani, wanatarajiwa kushuka tena dimbani kesho, kumenyana na Lipuli ya Iringa katika mfululizo wa Ligi Kuu, ikiwania kuendeleza rekodi yake nzuri. 
    Azam FC ambayo itaendelea kuwakosa wachezaji wake wawili majeruhi wa muda mrefu, winga Joseph Kimwaga na mshambuliaji Shaaban Iddi, kesho itacheza kwa mara ya tatu mfululizo nyumbani Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
    Azam FC inayodhaminiwa na Maji ya kunywa ya Uhai, Benki ya NMB na Tradegents, katika mechi zake za awali, ilishinda mara 1-0 mara mbili dhidi ya Ndanda FC mjini Mtwara na dhidi ya Kagera Sugar katikati ya sare ya 0-0 na Simba Uwanja wa Azam Complex. Lipuli ina pointi tano baada ya sare mbili na ushindi wa mechi moja.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAJIVUNIA REKODI YA KUTOFUNGIKA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top