• HABARI MPYA

  Friday, September 22, 2017

  LIGI KUU KUENDELEA KESHO, MWADUI KUPOZA MACHUNGU KWA PRISONS?

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MWADUI FC ya Shinyanga itajiuliza kwa Tanzania Prisons kesho katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ikitoka kuchapwa mabao 3-0 na Simba SC mjini Dar es Salaam wiki iliyopita.
  Mwadui wataikaribisha Tanzania Prisons Uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga katika mfululizo wa Ligi Kuu, wakati mabingwa watetezi, Yanga SC watakuwa wenyeji wa Ndanda FC ya Mtwara.
  Mchezo mwingine, utakutanisha timu za Majimaji itakayokuwa mwenyeji wa Njombe Mji kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea. Mechi zote hizo zitaanza saa 10.00 jioni.
  Jumapili Septemba 24, mwaka huu kutakuwa na michezo minne ambako Ruvu Shooting itaialika Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani huku Stand United ikicheza na Mbeya City kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga. Mechi hizo pia zitaanza saa 10.00 jioni.
  Michezo mingine itakuwa ni Singida United itakayoialika Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma saa 10.00 jioni kabla ya Azam kuialika Lipuli ya Iringa kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi katika mchezo utakaoanza saa 1.00 jioni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIGI KUU KUENDELEA KESHO, MWADUI KUPOZA MACHUNGU KWA PRISONS? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top