• HABARI MPYA

  Friday, September 22, 2017

  NEYMAR, MESSI, RONALDO KUWANIA MWANASOKA BORA WA FIFA

  FIFA imetaja washindani watatu wa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kiume wa Mwaka ambao ni Muargentina Lionel Messi, Mreno Cristiano Ronaldo na Mbrazil Neymar Junior ambaye ni ingizo jipya akichukua nafasi ya Mfaransa Antoine Griezmann.
  Majina hayo yametajwa leo mjini London, na Roberto Di Matteo, Jay Jay Okocha, na gwiji wa England, Peter Shilton wamekuwa miongoni mwa wachezaji wa zamani waliohudhuria hafla iliyofanyika ukumbi wa The Bloomsbury Ballroom, London.
  Wageni wengine waliohudhuria ni pamoja na beki wa timu ya wanawake ya Arsenal, Alex Scott na mshindi wa mwaka 2004, Andre Shevchenko, wakati sherehe zenyewe za tuzo zitafanyika mwezi ujao.

  Mbrazil Neymar Junior ameingia badala ya Mfaransa Antoine Griezmann aliyeingia tatu mwaka jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA


  Tuzo nyingine zinazotarajiwa kutolewa ni Mwanasoka Bora wa Kike, Kocha Bora wa Kiume, Kocha Bora wa Kike, Kipa Bora, Bao Bora la Mwaka maarufu kama tuzo ya Puskas sambamba na tuzo ya shabiki bora.
  Mshindi wa mwaka jana wa tuzo Wanaume, Ronaldo anapewa nafasi kubwa ya kushinda tena tuzo hiyo baada ya kuisaidia Real Madrid kutwaa mataji ya La Liga na Ligi ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita, hivyo anafukuzia tzo ya pili mfululizo mwaka huu, wakati mpinzani wake wa Barcelona, Lionel Messi anawania tuzo ya kwazna ya Mchezaji Bora wa FIFA.
  Gianluigi Buffon, Keylor Navas na majeruhi Manuel Neuer wameingia katika tatu upande wake wa makipa huku wengi wakitaka na kipa Manchester United, David De Gea ajumuishwe.
  Zinedine Zidane anawania kuwa mtu wa kwanza kushinda tuzo hiyo Mchezaji Bora na Kocha Bora wa FIFA akichuana na kocha wa Chelsea, Antonio Conte na Massimilliano Allegri wa Juventus.
  Manchester City ina mwakilishi mmoja tu, ambaye ni mshindi wa Kombe la Dunia na Medali mbili za Dhahabu za Olimpiki akiwa na Marekani, Carli Lloyd kuingia kwenye kinyang'anyiro cha tuzo ya Wanawake.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NEYMAR, MESSI, RONALDO KUWANIA MWANASOKA BORA WA FIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top