• HABARI MPYA

  Friday, September 29, 2017

  MECHI YA SUPERSPORT NA CLUB AFRICAIN YASOGEZWA MBELE

  SHIRIKISHO SHIRIKISHO  la Soka Afrika (CAF) limesogeza mbele kwa siku moja Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho baina ya SuperSport United ya Afrika Kusini na Club Africain ya Tunisia kutoka Jumamosi hadi Jumapili.
  Mchezo huo sasa utafanyika Uwanja wa Lucas 'Masterpieces' Moripe mjini Pretoria Jumapili ya Oktoba 1 kutokana na sababu za kiufundi, zilizosababisha msafara wa wageni kutuoka Tunisia uchelewe kufika Afrika Kusini.
  Wakitoka kuitoa Zesco United ya Zambia kwa mabao ya ugenini, SuperSport wana matumaini ya kuendeleza rekodi yao nzuri.
  SuperSport United wana matumaini ya kuendeleza rekodi yao nzuri Kombe la Shirikisho Afrika

  Walianza kwa sare ya 0-0 nyumabi, kabla ya kwenda kutoa sare ya 2-2 na Timh ya Ziko ugenini ambako kiungo, Thuso Phala alifunga mabao mawili mjini Ndola na anatarajiwa kuiongzoa timu yake tena dhidi ya Watunisia.
  Nusu Fainali nyingine ya michuano hiyo itazikutanisha TP Mazembe ya DRC na FUS Rabat ya Morocco Uwanja wa TP Mazembe mjini Lubumbashi Jumapili pia, wakati timu zote zitarudiana Oktoba 20, mwaka huu kusaka timu za kucheza fainali ya 2017.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MECHI YA SUPERSPORT NA CLUB AFRICAIN YASOGEZWA MBELE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top