• HABARI MPYA

    Tuesday, June 16, 2026

    VIUNGO WA MAGHARIBI WAFUNGA AZAM FC YAIGARAGAZA MASHUJAA 2-0 CHAMAZI


    TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Mabao yote ya Azam FC leo yamefungwa na viungo kutoka nchi za Magharibi mwa Afrika, Sadio Kanoute wa Mali dakika ya 39 na James Akaminko wa Ghana dakika ya 42. 
    Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 58 katika mchezo wa 27, ingawa inabaki nafasi ya tatu nyuma ya Simba SC yenye pointi 61 na mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 63 baada ya vigogo hao wote kucheza mechi 26 hadi sasa.
    Kwa upande wao Mashujaa FC baada ya kupoteza mchezo huo wanabaki na pointi zao 27 za mechi 27 nafasi ya 11 kwenye Ligi Kuu ambayo inashirikisha jumla ya timu 16 na mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja.
    Timu nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.    

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: VIUNGO WA MAGHARIBI WAFUNGA AZAM FC YAIGARAGAZA MASHUJAA 2-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top