• HABARI MPYA

  Sunday, November 19, 2023

  TANZANITE YATUPWA NJE KUFUZU KOMBE LA DUNIA WANAWAKE U20


  TIMU ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite imetupwa nje ya mbio za kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Colombia baada ya kufungwa mabao 2-1 na wenyeji, Nigeria leo katika mchezo wa marudiano Raundi ya Tatu kufuzu Uwanja wa Taifa wa Moshood Abiola Jijini Abuja.
  Kwa matokeo hayo, Tanzanite inaaga kwa kichapo cha jumla cha 3-2 kufuatia sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANITE YATUPWA NJE KUFUZU KOMBE LA DUNIA WANAWAKE U20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top