• HABARI MPYA

  Thursday, November 16, 2023

  TAIFA STARS WAENDA MOROCCO KUANZA MAWINDO YA TIKETI YA KOMBE LA DUNIA 2026


  TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeondoka leo kwenda Morocco kwa ajili ya mchezo wake wa kwanza wa Kundi E kufuzu Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2026 zinazoandaliwa kwa pamoja na nchi za Canada, Mexico na Marekani.
  Taifa Stars watakuwa wageni wa Niger Jumamosi Uwanja Marrakech nchini Morocco, kabla ya kuwakaribisha Morocco katika mchezo wa pili wa Kundi hilo Novemba 21, mwaka huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Pamoja na Taifa Stars, Niger na Morocco timu nyingine zilizopo Kundi E ni Kongo  na Zambia, wakati Eritrea imejitoa.
  Timu tisa zitakazoongoza makundi zitafuzu moja kwa moja kuiwakilisha kwenye Fainali za Kombe la Dunia, wakati washindi wa pili bora wanne wa makundi watamenyana katika Nusu Fainali na Fainali na mshindi atakwenda kushiriki mchujo wa Mabara kuwania nafasi ya kwenda Kombe la Dunia pia.
  Mchujo wa Mabara, unaojulikana kama Inter-Confederation Play-Offs ni michuano mingine midogo inayoshirikisha timu sita za Mabara manne duniani, kasoro UEFA pamoja na nchi mwenyeji kutoka CONCACAF kutafuta timu mbili za mwisho za kushiriki michuano hiyo.
  VIDEO: TAIFA STARS WALIVYOONDOKA LEO KWENDA MOROCCO 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS WAENDA MOROCCO KUANZA MAWINDO YA TIKETI YA KOMBE LA DUNIA 2026 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top