• HABARI MPYA

  Saturday, November 25, 2023

  YANGA YAANZA VIBAYA MAKUNDI, YACHAPWA 3-0 ALGERIA


  MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC wameanza vibaya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuchapwa mabao 3-0 na wenyeji, CR Belouizdad usiku huu Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers nchini Algeria. 
  Mabao ya CR Belouizdad katika mchezo huo wa Kundi D yamefungwa na kiungo Abdelraouf Benguit dakika ya 10 na washambuliaji, Abderrahmane Meziane Bentahar dakika ya 45 na ushei na Mgambia Lamin Jallow dakika ya 90 na ushei.
  Mechi nyingine ya Kundi D itachezwa kesho baina ya wenyeji, Al Ahly dhidi ya Medeama Ghana Uwanja wa Al Ahly Jijini Cairo nchini Misri.
  Yanga watashuka tena dimbani Desemba 2 kumenyana na mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam na CR Belouizdad watasafiri hadi Ghana kucheza na Medeama.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAANZA VIBAYA MAKUNDI, YACHAPWA 3-0 ALGERIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top