• HABARI MPYA

  Saturday, November 11, 2023

  MBEYA KWANZA YAREJEA KILELENI LIGI YA NBC CHAMPIONSHIP


  TIMU ya Mbeya Kwanza imefanikiwa kurejea kileleni mwa Ligi ya NBC Championship baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Stand United leo Uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga.
  Ushindi huo unawafanya Mbeya Kwanza wafikishe pointi 23, moja zaidi ya TMA ambayo leo imetoa sare ya 1-1 na Polisi Tanzania Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha hivyo inahamia nafasi ya pili baada ya wote kucheza mechi 10.
  Mechi nyingine za leo, Biashara United imeichapa Ruvu Shooting mabao 3-0 Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma na Cosmopolitan imetoa sare ya 1-1 na Green Warriors Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Ikumbukwe jana Mbeya City iliikanda Pamba FC mabao 2-1 Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Kesho kutakuwa na mechi tatu; Mbuni FC dhidi ya Fountain Gate Talents Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha, Copco na Ken Gold Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza na Pan Africans dhidi ya Transit Camp Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA KWANZA YAREJEA KILELENI LIGI YA NBC CHAMPIONSHIP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top