• HABARI MPYA

  Sunday, November 19, 2023

  SIMBA SC YAITANDIKA DAR CITY 4-0 WACAMEROON WOTE WAFUNGA


  TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Dar City ya Daraja la Kwanza katika mchezo wa kirafiki asubuhi ya leo Uwanja wa Mo Arena, Bunju Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba SC katika mchezo huo wa kujiandaa na hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika yamefungwa na Wacameroon, beki Che Malone Fondoh na kiungo mshambuliaji Leandre Willy Essomba Onana, beki mzawa Israel Patrick Mwenda na mshambuliaji Mzambia, Moses Phiri.
  Simba itateremka Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam Jumamosi kumenyana na ASEC Mimosas ya Ivory Coast katika mchezo wake wa kwanza wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Wakati huo huo, mchezaji wa timu hiyo, Mohamed Mussa amefiwa na baba yake mzazi, Mussa Mzee Saleh aliyefariki Dunia mapema leo visiwani Zanzíbar na anatarajiwa kuzikwa baada ya sala ya Alaasir huko Malindi.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAITANDIKA DAR CITY 4-0 WACAMEROON WOTE WAFUNGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top