• HABARI MPYA

  Saturday, November 25, 2023

  SIMBA SC YAANZA NA SARE YA NYUMBANI, 1-1 NA ASEC DAR


  WENYEJI, Simba SC wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na ASEC Mimosas ya Ivory Coast katika mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika leo Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Ni Simba SC waliotangulia na bao la penalti la kiungo wa Kimataifa wa Burundi, Saido Ntibanzokiza dakika ya 44, kabla ya mshambuliaji Muivory Coast, Serge N'guessan Archange Pokou kuisawazishia ASEC Mimosas dakika ya 77 akimtungua kipa Mmorocco, Ayoub Lakred.
  Mechi nyingine ya Kundi B itafuatia baadaye Saa 4:00 usiku baina ya wenyeji, Wydad Athletic Club na Jwaneng Galaxy ya Botswana Uwanja wa Marrakech Jijini Marrakech nchini Morocco.
  Simba SC itateremka tena dimbani Desemba 2 Uwanja wa Francistown Jijini Francistown nchini Botswana kumenyana na wenyeji, Jwaneng Galaxy wakati ASEC Mimosas watakuwa nyumbani siku hiyo kuwakaribisha Wydad Casablanca Uwanja wa Félix Houphouët-Boigny Jijini Abidjan.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAANZA NA SARE YA NYUMBANI, 1-1 NA ASEC DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top