• HABARI MPYA

  Wednesday, November 22, 2023

  KAGERA SUGAR YAAMBULIA SARE TU KWA KMC 1-1 KAITABA


  WENYEJI, Kagera Sugar wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Kagera Sugar walitangulia na bao la beki wake Mganda, Deus Bukenya dakika ya 49, kabla ya mshambuliaji Waziri Junior Shentembo kuisawazishia KMC dakika ya 74.
  Kwa matokeo hayo, KMC inafikisha pointi 16 na kupanda nafasi ya nne, wakati Kagera Sugar sasa ina jumla ya pointi 13 na inasogea nafasi ya saba baada ya wote kucheza mechi 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR YAAMBULIA SARE TU KWA KMC 1-1 KAITABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top