• HABARI MPYA

  Thursday, November 30, 2023

  MAN UNITED YAAMBULIA SARE KWA UTURUKI 3-3 NA GALATASARAY


  WENYEJI, Galatasaray usiku wa Jumatano wametoka sare ya kufungana mabao 3-3 na Manchester United katika mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Rams Global Jijini Istanbul nchini Uturuki.
  Mabao ya Manchester United tayari yamefungwa na Alejandro Garnacho dakika ya 11, Bruno Fernandes dakika ya 18 na Scott McTominay  dakika ya 55, wakati la Galatasaray yamefungwa na Hakim Ziyech dakika ya 29 na 62 na Kerem Akturkoglu dakika ya 71.
  Kwa matokeo hayo, Galatasaray wanafikisha pointi tano, sawa na FC Copenhagen ya Denmark, wakiwa nyuma ya Bayern Munich ambayo imekwishafuzu 16 Bora kwa pointi zake 13 na Manchester United yenye pointi nne inashika.
  Sasa Manchester United italazimika kuifunga Bayern Munich katika mchezo wa mwisho wa Kundi A na kuomba sare baina ya Galatasaray na FC Copenhagen ili iende 16 Bora.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAAMBULIA SARE KWA UTURUKI 3-3 NA GALATASARAY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top