• HABARI MPYA

  Sunday, November 19, 2023

  KWA KIASI KIKUBWA MAFANIKIO YA YANGA YAMETOKANA NA GSM - HERSI


  RAIS wa Yanga, Hersi Ally Said amesema kwamba mafanikio ya klabu hiyo kwa Asilimia 80 yametokana na msaada wa mfadhili na mdhamini mwenza wa klabu hiyo, Ghalib Said Mohamed ‘GSM’.
  Hersi ameyasema hayo leo wakati wa kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Ghalib ambayo ameifanyia katika hospitali ya Ocean Road na kutoa msaada wenye thamani ya Shilingi Milioni 137. 
  “Mafanikio ya klabu ya Yanga SC kwa zaidi ya asilimia 80 yamechangiwa na uwepo na Ghalib Said Mohamed. Tunamshukuru sana GSM yeye pamoja na familia yake. Ametutoa mbali sana na tunaendelea kumsihi aendelee kuinga mkono klabu hii. Nasi tutamuombea katika kila hatua kwenye maisha yake,” amesema Hersi na kuongeza;
  “Leo ni siku maalumu ya kuzaliwa kwa GSM. Siku hii angeweza kusheherekea kwa namna tofauti, lakini kwa mapenzi aliyo nayo kwa jamii ameona thamani ya kusheherekea na wenyewe uhitaji,”.
  Katika hafla hiyo GSM ametoa msaada wenye thamani ya Shilingi Milioni 137, wazo ambalo limetolewa mke wake Salha.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KWA KIASI KIKUBWA MAFANIKIO YA YANGA YAMETOKANA NA GSM - HERSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top