• HABARI MPYA

    Sunday, November 05, 2023

    YANGA YAWAFUNGA MDOMO KABISAA SIMBA SC, YAWATANDIKA 5-1 MAXI BALAA


    MABINGWA watetezi, Yanga SC wamewaadhibu ipasavyo watani wa jadi, Simba kwa kuwatandika mabao 5-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
    Mabao ya Yanga leo yamefungwa na mshambuliaji Mzambia, Kennedy Musonda dakika ya tatu na viungo, Mkongo Maxi Mpia Nzengeli dakika ya 64 na 77, Mburkinabe Stephane Aziz Ki dakika ya 73 na Muivory Coast Pacome Zouazoua dakika ya 87 kwa penalti.
    Refa Ahmad Arajiga wa Manyara alitoa adhabu ya penalti baada ya beki Mkongo, Henock Inonga Baka ‘Varane’ kumchezea rafu Nzengeli kwenye boksi na bao pekee la Simba limefungwa na Kibu Dennis Prosper dakika ya tisa.
    Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 21 katika mchezo wa nane na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu, ikiizidi pointi mbili Azam FC ambayo pia imecheza mechi moja zaidi.
    Kwa upande wao, Simba SC baada ya kipigo hicho cha kihistoria, inabaki na pointi zake 18 za mechi saba nafasi ya tatu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA YAWAFUNGA MDOMO KABISAA SIMBA SC, YAWATANDIKA 5-1 MAXI BALAA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top