• HABARI MPYA

  Thursday, November 30, 2023

  COASTAL UNION YAIKANDA GEITA GOLD 3-1 MKWAKWANI


  WENYEJI, Coastal Unión wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Geita Gold ilitangulia kwa bao la Valentino Mashaka dakika ya 12, kabla ya Coastal Unión kutoka nyuma kwa mabao ya kiungo Mbenin, Roland Junior Beakou dakika ya 30, Maabad Maulid dakika ya 53 na Charles Semfuko dakika ya 59.
  Kwa ushindi huo, Coastal Unión inafikisha pointi 13 na kusogea nafasi ya tisa, sawa na Geita Gold inayoshukia nafasi ya 10 baada ya wote kucheza mechi 12.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COASTAL UNION YAIKANDA GEITA GOLD 3-1 MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top