• HABARI MPYA

  Saturday, November 04, 2023

  AZAM FC YAIBATUA IHEFU SC 3-1 UBARUKU


  TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji, Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Highland Estate, Mbarali mkoani Mbeya.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na viungo Feisal Salum Abdallah dakika ya 15 na Sospeter Bajana mawili dakika ya 46 na 48, wakati la Ihefu SC limefungwa na Jaffary Kibaya dakika ya 90.
  Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 19 katika mchezo wa tisa na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu, ikizizidi pointi moja moja, Yanga iliyocheza mechi saba na Simba mechi sita, wakati Ihefu SC inabaki na pointi zake nane za mechi tisa nafasi ya 11.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAIBATUA IHEFU SC 3-1 UBARUKU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top