• HABARI MPYA

  Wednesday, November 29, 2023

  MAN CITY YATOKA NYUMA NA KUICHAPA RB LEIPZIG 3-2 ULAYA


  WENYEJI, Manchester City jana wametoka nyuma kwa mabao mawili na kushinda 3-2 dhidi ya Rasen Ballsport Leipzig katika mchezo wa Kundi G Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  RB Leipzig walitangulia kwa mabao ya mshambuliaji wake Mbelgiji, Ikoma-Lois Openda dakika ya 13 na 33, kabla ya Manchester City kutoka nyuma kwa mabao ya nyota, Mnorway Erling Haaland dakika ya 54, Muingereza Phil Foden dakika ya 70 na Muargentina Julián Álvarez dakika ya 87.
  Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 15 na kuendelea kuongoza Kundi G kwa pointi sita zaidi ya RB Leipzig wanaofuatia baada ya wote kucheza mechi tano kuelekea mechi za mwisho za makundi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YATOKA NYUMA NA KUICHAPA RB LEIPZIG 3-2 ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top